ChipuaAnza bure kwenye WhatsApp

Rekodi zako ni zako

Imesasishwa 28 Novemba 2026

Sisi ni nani

Chipua inaendeshwa na Upeosoft Limited, kampuni ya Kenya. Unaweza kutufikia wakati wowote kwenye WhatsApp: +254 725 307 131.

Chipua inahifadhi nini

Namba yako ya WhatsApp, ikiwa imesimbwa. Tunapata akaunti yako kwa msimbo wa namba, si kwa namba yenyewe.

Unachotuambia kuhusu duka: jina, aina, eneo na saa ya kufunga.

Ujumbe unaotuma ili Chipua iweke hesabu zako: maandishi, voice notes, picha za risiti za supplier na statement za M-Pesa, na rekodi zinazotokana nazo.

Tunahifadhi kwa muda gani

Faili za statement ya M-Pesa zinafutwa mara tu zinaposomwa. Password ya statement inatumika mara moja na haihifadhiwi.

Voice notes zinafutwa siku 90 baada ya kugeuzwa kuwa maandishi.

Rekodi za mauzo, matumizi na stock zinabaki muda wote unaotumia Chipua, ili ripoti zako ziwe sahihi.

Nani anaweza kuona

Wewe. Chipua haiuzi rekodi zako kamwe.

Mkopeshaji anaona muhtasari wa biashara yako tu ukikubali mkopeshaji huyo, na unaweza kuondoa ruhusa hiyo wakati wowote.

Ili ifanye kazi, Chipua inatumia watoa huduma: ujumbe wa WhatsApp, huduma ya AI inayosoma ujumbe na risiti zako, huduma ya kugeuza sauti kuwa maandishi, na Paystack kwa malipo ya usajili. Wanashughulikia data yako kwa ajili ya Chipua tu.

Chaguo zako

Tuombe kwenye WhatsApp kuona, kurekebisha au kufuta rekodi zako, nasi tutafanya hivyo. Unaweza kuacha kutumia Chipua wakati wowote.